
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akifanya mazungumzo na Shirikisho la Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kati
(ACEAC) kwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Rwanda,
wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhashamu Askofu José Moko Ikulu Jijini
Dar es Salaam tarehe 26 Feburari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Baraza la Maaskofu
Katoliki Afrika ya Kati (ACEAC) kwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Burundi na Rwanda, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhashamu Askofu
José Moko mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
tarehe 26 Feburari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akiagana na Viongozi wa Shirikisho la Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kati
(ACEAC) kwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Rwanda, mara
baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Feburari
2025.
………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Shirikisho la Baraza la Maaskofu
Katoliki Afrika ya Kati (ACEAC) linalojumuisha nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, Burundi na Rwanda, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhashamu
Askofu José Moko.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 26 Februari
2025 yamelenga kujadili namna ya kutafuta amani katika mgogoro unaoendelea mashariki
mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Post a Comment