" MBUNGE KATAMBI AENDELEA NA ZIARA KATA ZA NGOKOLO NA IBINZAMATA, AKABIDHI BASKELI KWA WATU WENYE ULEMAVU

MBUNGE KATAMBI AENDELEA NA ZIARA KATA ZA NGOKOLO NA IBINZAMATA, AKABIDHI BASKELI KWA WATU WENYE ULEMAVU

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Paschal Patrobas Katambi, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Februari 27, 2025.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Paschal Patrobas Katambi, ameendelea na ziara yake ya kutembelea kata mbalimbali za jimbo hilo, ambapo leo amefanya ziara katika kata ya Ngokolo na Ibinzamata.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Ngokolo, Katambi amekabidhi baiskeli za magurudumu matatu kwa watu wenye ulemavu, akiwemo mwanamke mmoja ambaye kwa zaidi ya miaka saba hajawahi kutoka nje ya nyumba yake.

Aidha Akiwa katika ziara hiyo, Katambi ameendelea kueleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha miaka minne, huku akiahidi kuendelea kutatua kero zilizobaki.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Ngokolo, Mhe. Victor Mkwizu, amesema zaidi ya shilingi bilioni moja zimetumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo:

Amesema zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule za msingi na sekondari, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa, vyoo, viti na meza pia amesema zaidi ya milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa soko la mitumba, choo cha soko la mitumba, na stendi ndogo mpya katika eneo hilo.

Pia Uboreshaji wa miundombinu ya barabara, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mitaro, madaraja, kalvati, na kuweka vifusi katika barabara zilizoharibika.

Mradi wa urasimishaji ardhi, hususan kwa mitaa ya Majengo Mapya, Mageuzi, Kalonga na Mwadui, ambapo wananchi wamehimizwa kufika ofisi za serikali za mitaa ili kupata hati miliki za viwanja vyao.

Baadhi ya wakazi wa Ngokolo wametumia fursa hiyo kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili,  huku wataalam kutoka taasisi husika wakiahidi kuzifanyia kazi.

Miongoni mwa kero zilizotolewa ni pamoja na Bili za maji kutoka SHUWASA na usomaji wa mita ambapo Angel Mwaipopo kutoka SHUWASA ameahidi kufuatilia suala hilo ili kuhakikisha wananchi hawalipishwi gharama zisizoeleweka.

Ubovu wa miundombinu ya barabara ambapo Mwakilishi wa TARURA ameeleza kuwa changamoto hizo zipo kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025, hivyo wananchi wametakiwa kuwa na subira.

Changamoto ya urasimishaji wa ardhi ambapo Mwakilishi wa Idara ya Ardhi amekiri kuwa bado kuna maeneo ambayo hayajarasimishwa, lakini zoezi hilo linaendelea na wananchi wametakiwa kujiandikisha kwa ajili ya kupatiwa hati miliki lakini pia Malipo ya fidia kwa wananchi na kwamba ameahidi kufuatilia malalamiko ya wananchi ambao hawajalipwa fidia na kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa ipasavyo.

Huduma duni hospitalini baadhi ya wananchi wamedai kuwa baadhi ya wahudumu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wamekuwa wakitoa lugha zisizo na staha kwa wagonjwa ambapo Katambi ameahidi kushughulikia suala hilo ndani ya siku nne.

Akihitimisha mkutano huo, Katambi amewahakikishia wananchi kuwa ataendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kutatua changamoto zinazowakabili.

"Nawahakikishieni kuwa mimi mbunge wenu, msiwe na shaka kabisa. Nitahakikisha changamoto zenu zinashughulikiwa. Tunataka kufanikisha lengo la Shinyanga kuwa jiji, na ili tufikie hapo, ni lazima tubadilishe mji wetu kwa maendeleo endelevu," alisema Katambi.

Katika mkutano huo, viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe, wamehudhuria.

 

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Paschal Patrobas Katambi, awali akizungumza kwenye kikao cha ndani Februari 27, 2025.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Paschal Patrobas Katambi, awali akizungumza kwenye kikao cha ndani Februari 27, 2025.

 



 

Post a Comment

Previous Post Next Post