Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga imekabidhi cheti cha pongezi kwa MISALABA MEDIA kwa mchango wake mkubwa katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria na Siku ya Sheria kwa mwaka 2025.
Hafla ya utoaji wa vyeti hivyo imefanyika Februari 6, 2025, ikiwa ni ishara ya kuthamini juhudi za wadau mbalimbali waliowezesha mafanikio ya maadhimisho hayo. MISALABA MEDIA imetambuliwa kwa mchango wake wa kipekee katika kuhabarisha jamii kuhusu shughuli za mahakama na kuimarisha uhusiano kati ya Mahakama na wananchi.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa MISALABA MEDIA kupokea cheti hiki, baada ya kutambuliwa katika maadhimisho ya mwaka jana. Tuzo hii inaonesha namna chombo hiki cha habari kinavyoendelea kuwa sehemu muhimu ya kuelimisha na kuhabarisha umma kuhusu masuala ya sheria na haki.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Frank Habibu Mahimbali, ameeleza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kuhakikisha wananchi wanapata uelewa kuhusu sheria na haki zao.
MISALABA MEDIA inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha taarifa sahihi zinawafikia wananchi kwa wakati na kwa ufanisi.
Post a Comment