" SHINYANGA WAADHIMISHA WIKI YA MARIDHIANO

SHINYANGA WAADHIMISHA WIKI YA MARIDHIANO


Na Moshi Ndugulile 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julias Mtatiro amewaongoza wajumbe wa Jumuiya ya maridhiano na Amani Tanzania-JMAT Mkoa wa Shinyanga, kupanda miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho kuelekea siku ya maridhiano Nchini.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo wakili Mtatiro amewapongeza wajumbe wa jumuiya hiyo ya maridhiano na Amani kufanya maadhimisho kwa kushiriki katika shughuli hiyo ya kijamii, ambayo ni ajenda endelevu katika juhudi za kulinda na kutunza mazingira.

Wakili Mtatiro ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha amesema kuwa upandaji wa miti ni zoezi endelevu ambalo limelenga kutunza mazingira.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya maridhiano na Amani Sheikh Khamis Balilusa amesema Jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na serikali katika juhudi zote za kulinda Amani,umoja na mshikamano uliopo kwa maslahi mapana ya watanzania, na kuhakikisha migogoro inayojitokeza inapata suluhu kwa njia ya maridhiano.

 Kwa upande wake afisa msimamizi wa Idara ya maliasili na hifadhi ya mazingira katika manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga, amesema ofisi yake imeshiriki katika uratibu wa zoezi hilo la kupanda jumla ya miti 80 imepandwa nje ya eneo la ofisi ya mkuu wa wilaya pamoja na kwenye eneo la wazi lililopo mtaa wa Tambukaleli kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Kitaifa maadhimisho ya siku ya maridhiano na amani yatafanyika Mkoani Arusha na kwamba kilele chake ni Februari 26,2025 ambapo yanafanyika sanjari na kauli mbiu inayosema “Uchaguzi Huru wa Haki na Amani kwa maendeleo endelevu,tukatae udini”MWISHO






 
















Post a Comment

Previous Post Next Post