Na Sayi Mathias
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamring Macha amesema amelidhishwa na kilimo cha kisasa cha zao la pamba kinachotekelezwa na baadhi ya wakulima katika Vijiji vya Kata ya Ngofila Wilaya ya Kishapu .
Ameyabainisha hayo February 18,2025 wakati akikagua mashamba ya zao la pamba katika vijiji tofauti katika Kata hiyo kikiwemo Kijiji cha Ngofila na Mwamanoga ambapo amewashukuru wakulima kwa kuzingatia ushauli wa Maafsa Ugani kwani umeleta matokeo chanya ya zao hilo
Amesema kuwa anasikitishwa na uhaba wa dawa za kutibia mimea ya zao hilo hivyo akawataka wakulima kumpa siku chache ili kutatua changamoto hiyo.
‘’Suala la uhaba wa madawa ya kutibia mimea ni kitu ambacho kinanisikitisha kila ninapotembelea wakulima na siyo ninyi tu sasa mnipe siku ya leo na kesho nikalishughulikie ili siku mbili hizi dawa ipatikane’’amesema Rc Macha.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Niclous Masindi amewataka wakulima kuongeza maeneo ya mashamba hususani kuanzia hekali tano kwakufanya hivyo kutawasaidia kupata kipato kitakachowawezesha kukidhi mahitaji yao.
‘’Amewashukuru wakulima kwa jitihada munazozionesha lakini niwashauri ongezeni Zaidi maeneo ya mashamba mwenye heka moja ongeza mpaka heka tatu ,heka tano itawawezesha kujiingizia kipato kikubwa Zaidi’’amesema Dc Masindi .
Nao baadhi ya wakulima wa zao hilo akiwemo Esta Mwandu wa Kijiji cha Mwamanota na Jishuli Mathias Zengo wa Kijiji cha Ngofila wamesema kupitia kilimo cha zao la pamba wanawasomesha watoto wao na wanaendelea na ujenzi wa nyumba imara za blok na kuachana na nyumba za nyasi (tembe).
Mkakati wa Serikali ya Mkoa wa Shinyanga ni kuhakikisha mkulima anavuna kilo elfu moja miambili za pamba kwa heka moja.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Niclous Masindi akizungumza.
Post a Comment