Mkuu wa Shule ya Sumve Sekondari amepongeza mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi Cha Dkt Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Akizungumza Jana Mkuu wa Shule ya Sekondari Sumve Clotilda Elly amesema Shule ya Sekondari Sumve imekuwa Ikifanya vizuri katika mitihani mbalimbali ya kitaifa tangia kuingia madarakani Dkt Samia Suluhu Hassani kutokana na kuleta kwa fedha nyingi kwa ajili ya kujenga miundo mbinu ya shule ikiwa ni mabweni manne yenye uwezo wa kulaza wanafuzi 80 na matundu 16 ya vyoo.
Elly amesema kutokana na Kuboresha miundo mbinu ya Shule wanafunzi katika shule hiyo wanafanya vizuri ambapo hadi kidato cha nne wavulana ni 467 wasichana 1710 jumla 2,177 na vidayo vya juu school ina wanafunzi 778.
Post a Comment