
Na Ashrack Miraji
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amesikia kilio cha wananchi wa Bumbuli, mkoani Tanga kuhusu ujenzi wa barabara ya Soni – Bumbuli – Korogwe (km 77), kwa kiwango cha lami ambapo ameeleza kuwa ujenzi wa barabara hiyo utajengwa kwa awamu.
Akihutubia wananchi wa Wilaya ya Lushoto mkoani humo katika mkutano wa hadhara Februari, 24 2025 Rais Samia ameeleza kuwa tarehe 06 Machi, 2025 Serikali itafungua zabuni ya kumtafuta Mkandarasi wa kujenga barabara hiyo.
Dkt. Samia amesisitiza kuwa ujenzi wa barabara hiyo utaanzia Soni- Bumbuli (km 22) na Kwameta – Kwashemsi (Km 9.3).
“Barabara hii (Mbunge wa Bumbuli) amekuwa akiililia sana, baada ya kusikia kilio chake basi nikasema tangazeni, tarehe 6 mwezi ujao tunafungua tenda kutafuta mkandarasi,” amesema Dk. Samia.
Aidha, ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza ujenzi wa barabara ya Tanga – Pangani – Bagamoyo (km 218.2) kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa Daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525.
Mkuu wa wilaya ya Lushoto Zephania Sumaye ametumia fulsa hiyo kumpongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo ameifanya na anaendelea kuifanya kwa wananchi wa wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga
Mhe Rais nikuhakikishie tu Wananchi wa wilaya ya Lushoto wamehamua kuwasha taa ya kijani hasa kwa kazi kubwa ambazo umezifanya kwa kutuletea miradi mikubwa ya Maendeleo pia Leo wameshuhudia kwa macho Yao umetuwekea jiwe la Msingi ufunguzi wa jengo la Halmashauri ya bumbuli wilaya ya Lushoto kwa niaba ya wananchi nikiwa kama kiongozi wao hatuna budi kukushukuru alisema Sumaye
Sambamba na hayo Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba amemshukuru Rais Dk. Samia kwa kutoa kibali cha barabara hiyo kutangazwa ambayo itakuwa mkombozi na kiuganisha kati ya Bumbuli na Korogwe Mkoani Tanga.
Rais Dk.Samia anaendelea na ziara yake mkoani Tanga ambapo leo ameweka jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo la Halmashari ya wilaya ya Bumbuli na kuzungumza na wananchi wa wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.


Post a Comment