Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media
Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini "TCAA" imetoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa wafungwa na mahabusu wa Gereza Kuu la Karanga mjini Moshi - Kilimanjaro.
Misaada iliyotolewa gerezani hapo na "TCAA" Kwa wafungwa na mahabusu ni sabuni,taulo la kike"ped" pamoja na dawa meno.
Akizungumza wakati wa zoezi Hilo mkurugenzi mkuu wa "TCAA" Bw Salim Msangi amesema
“Kwa kweli niseme, taasisi zote binafsi, za serikali tuelewe tu kwamba tuna wajibu wa kuwasaidia hawa wafungwa ambao wako hapa kuna wafungwa na mahabusu ambao wanahifadhiwa hapa ambao wanahitaji huduma muhimu na serikali haiwezi kufanya kila kitu…," .
Sambamba na hilo amezitaka taasisi binafsi na serikali kuwa na utamaduni wakutembelea wafungwa na mahabusu katika magereza.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, SACP Leonard Burushi ameishukuru Mamlaka hiyo na kusema misaada hiyo imekuja kwa wakati muafaka.
Post a Comment