Na BelnardoCostantie, Misalaba Media
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi Tanzania "TPLB",imewapa Onyo kali viongozi wa klabu ya Yanga kufuatia kitendo cha kuingia Uwanjani katika eneo la kuchezea "Pitch Area" ,wakati wa mechi kati ya Yanga na Singida black Stars iliopigwa kwenye Uwanja wa "KMC" Mwenge ambapo yanga iliongoza Kwa ushindi wa magoli 2-1.
Taarifa hiyo imetoka leo ya ,Februari 23, 2025 na Kamati hiyo kufuatia kikao chake cha Februari 21, 2025 imeeleza kuwa viongozi hao wa klabu ya Yanga walioingia uwanjani walisababisha kukosekana kwa utulivu wakati wa mahojiano ya mdhamini mwenye haki za matangazo ya runinga.
Post a Comment