" VIONGOZI WA SMAUJATA SHINYANGA WAJADILI KONGAMANO LA WANAWAKE NA WANAWAKE WENYE ULEMAVU

VIONGOZI WA SMAUJATA SHINYANGA WAJADILI KONGAMANO LA WANAWAKE NA WANAWAKE WENYE ULEMAVU

Jumuiya ya Kupinga Ukatili nchini, Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga, inatarajia kufanya kongamano maalum la wanawake na wanawake wenye ulemavu.

Kongamano hilo limepangwa kufanyika Machi 1, 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Lyakale Hoteli, mjini Shinyanga.

Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma.

Katika hatua za maandalizi, baadhi ya viongozi wa SMAUJATA Shinyanga wamekutana leo kwa kikao cha pamoja ili kujadili masuala muhimu yatakayosaidia kufanikisha kongamano hilo.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga, Madam Nabila Kisendi, amesisitiza umuhimu wa mshikamano na ushirikiano kuelekea siku hiyo muhimu. 

Pia, amewakaribisha wananchi, viongozi wa serikali na wadau mbalimbali kushiriki katika kongamano hilo kwa wingi.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga, Madam Nabila Kisendi.


 


 

Post a Comment

Previous Post Next Post