Na Mapuli Kitina Misalaba
Viongozi wa Jumuiya ya Kupinga Ukatili nchini, SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga, leo wamekutana kwa kikao cha mwisho kama sehemu ya maandalizi ya kongamano la wanawake na wanawake wenye ulemavu linalotarajiwa kufanyika kesho.
Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili na kuweka mikakati ya mwisho ili kuhakikisha kongamano linafanikiwa kwa ufanisi.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga, Madam Nabila Kisendi, amesisitiza mshikamano na ushirikiano kati ya wanajumuiya na wadau wote katika kuhakikisha malengo ya kongamano yanatimia.
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Machi 1, 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Lyakale Hoteli, Shinyanga, ambapo Mhe. Riziki Pembe Juma, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Zanzibar, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
SMAUJATA imewataka wananchi, viongozi wa serikali, na wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushiriki kongamano hilo muhimu.
Safari ya Ladha: Ubora wa East African Spirits (T) Ltd
Post a Comment