Walimu wa Somo la kiingereza na Fasihi ya kiingereza (Literature) Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa mafunzo na mbinu ya kuongeza ufaulu kwa masomo hayo ikiwa ni juhudi ya serikali Katika kuboresha somo la kiingereza.
Akifungua mafunzo haya leo februari 17, 2024, mafunzo yatakayo fanyika kwa siku mbili 17 na 18 Februari , 2025 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Ndg. Charles Luchagula amesema mikakati ya Serikali ni kuboresha namna ya ufundishaji, Kuimarisha lugha ya kiingereza, Kuibua ushirikiano baina ya walimu wa somo la kiingereza.
“Mafunzo haya yasiwe bure ikawe mbegu kwa walimu wengine huko shuleni ili tuweze kuongeza ufaulu wa somo la kiingereza kwenye Halmashauri yetu, Somo la kiingereza ni Msingi wa mawasiliano duniani kote mikakati ya serikali ni kuboresha namna ya ufundishaji, mbinu ya Kuimarisha lugha ya kiingereza pamoja na Kuibua ushirikiano baina yenu walimu, nitumie fursa hii kuwapongeza walimu wote wa Manispaa ya Shinyanga kwa juhudi na ushindani mkubwa mlio nao kwa Mwalimu mmoja mmoja ndiyo maana katika mitihani ya kidato cha pili na nne tumefanya vizuri ”Amesema Ndg. Luchagula
Kwa upande wake Afisa Elimu Taaluma Sekondari Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Makoye Richard amesema Katika kutambua mchango wa walimu waliofanya vizuri pamoja na shule zilizofanya vizuri Katika mitihani ya kidato Cha nne 2024 uongozi wa Manispaa ya Shinyanga kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri umejipanga kuandaa Siku ya Tuzo ya walimu kwa lengo la Kuwatambua walimu waliofanya vizuri Katika masomo yao katika mtihani wa kidato cha nne, kwa kutambua jitihada zao na mchango wao Katika masomo mbalimbali kwa kila shule iliyofanya vizuri.
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika mtihani wa kidato cha pili imefanikiwa kupata ufaulu wa 87%. Huku kidato cha nne wanafunzi wamefaulu kwa 97% na kuifanya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kushika nafasi ya kwanza kimkoa kati ya halmashauri sita za mkoa huu.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya shinyanga aliye katikati ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha sanaa michezo na burudani Hakmashauri ya manispaa ya shinyanga ndg. Charles Luchagula
Afisa elimu taaluma halmashauri ya manispaa ya shinyanga mwl. Richard Makoye akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Post a Comment