
Mabingwa Watetezi Yanga SC wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara uliochezwa leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na washambuliaji mzawa Clement Francis Mzize dakika ya 14 na Mzimbabwe Prince Dube dakika ya 43, wakati bao la Singida Black Stars limefungwa na mshambuliaji Mghana Jonathan Sowah dakika ya 90 +2.
Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 52 katika mchezo 20 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tano zaidi ya watani wao Simba SC ambao pia wana mechi mbili mkononi, huku Singida Black Stars wanabaki na pointi 37 za mechi 20 nyuma ya Azam Fc yenye pointi 42 za mechi 19.
Post a Comment