Mkuu wa Shule ya Sekondari Kabale Masikitiko Lubela alitoa taarifa hiyo hivi karibuni kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa wilayani Kwimba akisema kuwa fedha hizo zimetolewa na Serikali kupitia mradi wa Sequip.
Alisema shughuli zinazofanywa kupitia mradi huo kuwa ni Ujenzi wa vyumba vinane vya madarasa na ofisi nne ambazo kwa sasa ziko katika hatua ya umaliziaji na jengo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Ikiwa vilevile kwenye hatua hiyo.
Vilevile aliongeza kusema kuwa Ujenzi mwingine unaofanywa ni wa Maktaba, Maabara ya Kemia, Fizikia na Biolojia ambapo ujenzi wake uko katika hatua za ujengaji wa meza na kufunga mfumo wa maji na ujenzi wa matundu 11 ya choo Ikiwa katika umaliziaji.