
Aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Chanika (OCD), Awadh Mohamed Chiko, amefariki dunia baada ya kupata ajali katika eneo la Gongolamboto Mwisho, kwenye kilima kinachoelekea Shule ya Sekondari Pugu.
Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo imetokea baada ya daladala aina ya Eicher kutanua na kuingia upande wa gari aina ya Toyota Prado, ambalo lilikuwa likiendeshwa na marehemu OCD Awadh, na kusababisha mgongano mkali.
Vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo huku hatua zaidi zikiendelea kuchukuliwa.
Post a Comment