KAIMU Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Caroline Damian akihitisha maadhimisho ya siku ya figo duniani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika viwanja vya Nyerere Square.

Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala UDOM Prof. Pendo Kasoga akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya figo duniani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika viwanja vya Nyerere Square.

Amidi wa Shule Kuu ya Uuguzi na Afya ya Jamii Dkt. Stephen Kibusi akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya figo duniani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika viwanja vya Nyerere Square.

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dodoma walio ungana na UDOM kuadhimisha ya siku ya figo duniani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika viwanja vya Nyerere Square.

Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Caroline Damian akiwa na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala UDOM Prof. Pendo Kasoga wakikagua huduma zinazotolewa kwenye mabanda wakati wa maadhimisho ya siku ya figo duniani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika viwanja vya Nyerere Square.

KAIMU Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Caroline Damian,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki katika maadhimisho ya siku ya figo duniani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika viwanja vya Nyerere Square.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Imeelezwa kuwa kati ya asilimia 7 mpaka 25 ya Waafrika wana changamoto ya ugonjwa sugu wa figo hususani nchi zinazoendelea huku ikiwa mara Tatu zaidi ya mataifa mengine kama hayo.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Caroline Damian wakati akihitisha maadhimisho ya siku ya figo duniani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), huku yakienda sambamba na utoaji wa huduma za afya kwenye viwanja vya Nyerere Square.
“Kwa nchi ya Tanzania takribani wagonjwa 4,300 ufariki kila mwaka kutokana na changamoto au magonjwa sugu yanayotokana na figo na hizi takwimu ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani,”amesema.
Amesema siku ya figo duniania ni kampeni ya kimataifa yenye lengo la kuongeza ufahamu unaohusu umuhimu wa kutunza figo ili kupunguza madhara yatokanayo na ugonjwa wa figo huku pia na wataalamu wa afya wakiwa wanapata fursa ya kufanya uhamasishaji kwa wananchi na jamii kwa ujumla.
Aidha, amewahasa wananchi ambao wamepima na kujigundua kuwa na magonjwa yanayosababisha ugonjwa figo ikiwemo kisukari na shinikizo la damu kuzingatia matumizi sahihi ya dawa.
“Pia, muhakikishe madhara au magonjwa hayo yanatibika na kuepuka madhara sugu yanayoweza kupelekea kuangamiza figo zetu na baadae kuleta changamoto kubwa japo tunafahamu gharama za huduma ya afya ni kubwa kwahiyo tunapokinga na kupata matibabu ya mapema na haraka basi tunazuia madhara ya magonjwa hayo mapema,”amesema.
Kwa upande wake Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala (UDOM), Prof. Pendo Kasoga amesema chuo hicho kinao utaratibu wa kila mwaka kufanya maadhimisho hayo ambayo ufanyika kila Alhamisi ya ya pili ya mwezi wa Tatu ikiwa ni njia ya kuungana na wadau wengine duniani katika kutoa hamasa na elimu ya juu ya afya ya figo.
“Kupitia kampeni hii jamii imeelimishwa na kuweza kujengewa uwezo wa jinsi ya kujizuia na magonjwa ya figo pamoja na kujua vitu vinavyosababisha na kuchangia kuongezeka kwa wagonjwa sugu wa figo,”amesema.
Prof. Kasonga ameongeza kuwa uchunguzi wa magonjwa ya figo unapaswa kuimarishwa zaidi nje na mazingira ya hospitali kama vile kambi, Makanisa, Masoko na hata Vijijini ili watu waweze kupata uelewa juu ya suala hilo.
Post a Comment