" BARAZA LA WATOTO MKOA WA SHINYANGA LASHIRIKI KATIKA KIKAO CHA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA KUTHIBITI UKATILI (MTAKUWA 2)

BARAZA LA WATOTO MKOA WA SHINYANGA LASHIRIKI KATIKA KIKAO CHA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA KUTHIBITI UKATILI (MTAKUWA 2)


Baraza la Watoto Mkoa wa Shinyanga limeendelea kusimamia haki na ustawi wa watoto kwa kushiriki katika kikao muhimu cha kuandaa Mpango Mkakati wa Kuthibiti Ukatili Mkoa wa Shinyanga (MTAKUWA 2). 

Kikao hiki kimefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, kikiandaliwa na Women Fund Tanzania Trust (WFTT) na WiLDAF Tanzania, kwa kushirikiana na serikali ya mkoa pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Baraza la Watoto limehusishwa kikamilifu kupitia Mwenyekiti Raphael Charles Joseph na Katibu Amina Khamis, wakibeba sauti za watoto wote wa Shinyanga katika kuhakikisha mpango huu unazingatia maslahi yao.

Katika kikao hicho, washauri waelekezi Dr. Juma Almasi na Annmarie Mavenjina waliwaongoza washiriki katika majadiliano ya makundi yaliyogawanywa kwenye thematic areas 8, ambazo ni:

1️⃣ Uboreshaji wa uchumi katika ngazi ya familia
2️⃣ Mila na desturi
3️⃣ Mazingira salama
4️⃣ Kuzuia ukatili
5️⃣ Sheria na mifumo ya kisheria
6️⃣ Huduma za msaada na mwitikio
7️⃣ Shule salama kwa wote

Baada ya majadiliano, kila kundi liliwasilisha mapendekezo yake, na kwa pamoja walijadili hatua bora za kutekeleza mpango huu kwa ufanisi.

Kwa niaba ya watoto wote wa Shinyanga, Baraza la Watoto lilitoa maoni na mapendekezo kuhusu namna bora ya kulinda haki za watoto, kuhakikisha mazingira salama kwao, na kuimarisha juhudi za kutokomeza ukatili katika jamii.






























































































































































Post a Comment

Previous Post Next Post