" BENKI YA CRDB YAENDELEA NA KAMPENI YAKE YA "TUPO MTAANI KWAKO" MKOANI SHINYANGA

BENKI YA CRDB YAENDELEA NA KAMPENI YAKE YA "TUPO MTAANI KWAKO" MKOANI SHINYANGA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Benki ya CRDB inaendelea na kampeni yake kubwa ya TUPO MTAANI KWAKO, ikilenga kuwafikia wananchi moja kwa moja kwa kutoa elimu kuhusu huduma zake, hususan LIPA HAPA, ambayo inawawezesha wafanyabiashara kupokea malipo kutoka benki na mitandao yote ya simu kwa urahisi.

Meneja wa Kanda ya Magharibi wa CRDB, Jumanne Wagana, amesema kampeni ya mwaka huu imepata mwitikio mkubwa na imepanuka zaidi kuliko miaka iliyopita. "Kampeni hii ni sehemu ya dhamira yetu ya kuwa karibu na wateja wetu. Tumejipanga kufika katika kila kona ya Shinyanga Manispaa na kisha kuendelea na safari yetu kuelekea Kahama na mikoa mingine ya Kanda ya Magharibi," amesema Wagana.

Msafara wa magari zaidi ya 10 umeshawasili Shinyanga, ukiwa na timu ya wataalamu wa CRDB waliopo tayari kusaidia wananchi kufahamu namna ya kutumia huduma za benki kwa ufanisi. "Tunahamasisha wafanyabiashara kutumia LIPA HAPA kwa kuwa ni huduma ya bure inayorahisisha upokeaji wa malipo ya kibenki na mitandao yote ya simu, hivyo kumpunguzia mteja usumbufu wa kubeba pesa taslimu," ameongeza Wagana

Wananchi wa Shinyanga wanahamasishwa kufuatilia msafara huu ili kupata huduma na maelezo ya kina kuhusu huduma za CRDB.

 Meneja wa Kanda ya Magharibi wa CRDB, Jumanne Wagana, akizungumza leo Machi 6, 2025.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post