Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa, ametangaza kuwa chama hicho kitaanza rasmi ziara ya mikutano ya hadhara nchi nzima kuanzia Machi 23, 2025.
Ziara hiyo itaanzia Kanda ya Nyasa, ambapo mkoa wa Mbeya utakuwa kituo cha kwanza cha mikutano hiyo.
Ametoa tangazo hilo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Machi 19, 2025, katika makao makuu ya CHADEMA jijini Dar es Salaam.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment