" MAKATIBU WASTAAFU WA CHADEMA TANZANIA WADAI STAHIKI ZAO

MAKATIBU WASTAAFU WA CHADEMA TANZANIA WADAI STAHIKI ZAO


DAR ES SALAAM: Baadhi ya makatibu wastaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nchini Tanzania wanadai kulipwa stahiki zao baada ya kuhudumu katika chama kwa miaka kadhaa.

Mmoja wao, Renatus Nzemo, aliyewahi kuwa Katibu wa Kanda ya Serengeti, ameshinda kesi ya madai dhidi ya CHADEMA baada ya mahakama kuamuru chama hicho kimlipe Shilingi 60,928,335.32. Nzemo, ambaye alihudumu katika kanda inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Simiyu, na Mara, aliwasilisha kesi mahakamani mwaka 2019 baada ya kuondolewa ofisini, akidai haki zake za kiutumishi.

Awali, madai yake yalifikia Shilingi milioni 100, lakini sasa mahakama imeamuru alipwe takriban milioni 60. Hatua hiyo imeibua mjadala miongoni mwa makatibu wengine wastaafu wa CHADEMA, ambao nao wanadai kulipwa haki zao kwa mujibu wa utaratibu wa chama.

Makatibu hao wanasisitiza kuwa walihudumu kwa muda mrefu ndani ya chama na wanapaswa kulipwa stahiki zao kama ilivyo haki yao.

Taarifa zaidi zinaendelea kufuatiliwa.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post