" DAR ES SALAAM YAONGOZA UZALISHAJI TAKA, KWA TANI LAKI NNE KWA MWEZI

DAR ES SALAAM YAONGOZA UZALISHAJI TAKA, KWA TANI LAKI NNE KWA MWEZI


Na Halima Issa, Misalaba Media 

Mkurugenzi Mkuu Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)Dkt. Immaculate Semesi ameeleza kuwa Jiji la Dar es salaam ndilo Jiji linaloongoza kwa uzalishaji wa taka ambapo kwa mwezi huzalishwa taka tani laki nne ambazo kwa asilimia kubwa ni taka za plastiki ambazo zimekuwa ni changamoto moto katika kuzitenganisha na zingine.

Ambapo Amesema siku za hivi karibuni NEMC wamesaini Makubaliano na moja ya Kampuni kutoka Uturuki ambayo ni Kampuni mahsusi katika mabadiliko yaTabianchi,ambapo kwa sasa wataweza kuchakata taka hasa plastiki ambazo hazimeng'enyeki,kwa kutafuta vikundi vya vijana,Taasisi au mtu binafsi kuzikusanya na kufanyiwa urejereshaji kwani kule Uturuki wao wanazitumia kwa kuzalisha umeme. 

Dkt Semisi ameeleza hayo mapema leo Jijini Dodoma Machi 24 Katika Mkutano wake na Wanahabari akielezea mafanikio na mwelekeo wa Taasisi hiyo katika Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.

"Dar es Salaam tu pekee inaongoza kwa kuzalisha taka ambapo tani laki 4 kwa mwezi huzalishwa,sasa hizo taka ukikuta asilimia kubwa ni plastiki ambazo haziwezi kufanyiwa kitu chochote,lakini pia tunahasishana sote tuwe na utaratibu wa kutenganisha taka yani taka hatarishi,zinazoweza kuwa mbolea na plastiki zinzoweza kufanyiwa urejeshaji".





Post a Comment

Previous Post Next Post