Hawa Halifani Mbega mkazi wa Mtaa wa Mnazi Mmoja Kata ya Jangwani Dar es Salaam akifurahia kadi yake mpya ya Mpiga Kura baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele. Mkoa wa Dar es Salaam umeanza leo uboreshaji wa Daftari na utadumu kwa siku saba hadi Machi 23 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele akimkabidhi kadi mpya ya Mpiga Kura Ndg. Hawa Halifani Mbega mkazi wa Mtaa wa Mnazi Mmoja Kata ya Jangwani Dar es Salaam ambaye alijitokeza wa kwanza kujiandikisha katika kituo cha Shule ya Msingi Mnazi. Mkoa wa Dar es Salaam umeanza leo uboreshaji wa Daftari na utadumu kwa siku saba hadi Machi 23 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo Machi 17, 2025 ametembelea baadhi ya vituo vya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Dar es Salaam na kushuhudia mwenendo wa zoezi hilo katiuka siku ya kwanza. Mkoa wa Dar es Salaam umeanza leo uboreshaji wa Daftari na utadumu kwa siku saba hadi Machi 23 mwaka huu.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk leo Machi 17, 2025 ametembelea vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
***************
Na. Mwandishi Wetu
Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaa wameanza
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo wananchi wengi walionekana
kwa wingi vituoni kujiandikisha au kuboresha taarifa zao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Machi 17, 2025 baada ya kutembelea vituo vya Uboreshaji, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele alisema zoezi hilo limeanza vyema pasi na changamoto yeyote na kuwataka wananchi kuendelea kujitokeza.
“Tume inaendelea na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na sasa tupo mzunguko wa 13 mkoani Dar es Salaam, nimeshuhudia kuanza kwa zoezi katika kituo cha Mnazi Mmoja…watu wengi wamejitokezakuja kujiandikisha na kuboresha taarifa zao,”alisema Mhe. Jaji wa Rufani Mwambegele.
Jaji wa Rufani Mwambegele amesema mwitikio wa wananchi ni mkubwa na ameshauri wananchi wa Dar es Salaam kuzitumia siku za mwanzo za uboreshaji ili kuepusha msongamano kwa siku za mwishoni mwa zoezi.
“Nawasihi watanzania wale wanaostahili wajitokeze kwa wingi kuja kuboresha taarifa zao au kujiandikisha, leo tarehe 17 mwezi huu wa tatu, 2025 ndio siku ya kwanza mwisho tarehe 23 mwezi huu wa tatu 2025 sasa tunakawaida ya kusubiri siku za mwisho hivyo nawasihi waje siku hizi za mwanzo,” alisema Jaji Rufaa Mwambegele.
Nae Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yenye Majimbo ya Kawe na Kinondoni Ndg. Omary Mkangama amesema zoezi hilo limeanza vizuri na hali ni shwari na wananchi wanapata huduma vizuri.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inataraji kuandikisha Wapiga Kura wapya 643,420 mkoani Dar es Salaam ambapo jumla ya vituo 1,757 vinatumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 96 katika vituo 1,661 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.
Aidha Tume imejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wote wenye sifa za kuandikishwa wanaandikishwa kwani BVR zaidi ya 5,000 na watendaji wa kutosha wapo kwaajili ya utekelezaji wa zoezi hilo.
Tume imeshakamilisha uboreshaji wa Daftari katika Mikoa 29. Kwa mujibu wa ratiba, leo Tume inaanza uboreshaji katika mzunguko wa 13 ambao ni mzunguko wa mwisho wa uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu unahusisha Mkoa wa Dar es Salaam pekee.
Kailima amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 643,420 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 3,427,917 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa na wapiga kura 4,071,337 idadi ambayo inaweza kuongezeka kwa kuwa inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza kujiandikisha.
Zoezi la uboreshaji wa Daftari linahusu kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine.
Uboreshaji wa Daftari pia unahusu kutoa fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye Daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au jimbo walipoandikishwa awali na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania na kifo.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri leo tarehe 17 Machi, 2025 ametembela vituo mbalimbali vya kuandikisha Wapiga kura vya Jimbo la Kibamba Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam kuona zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linavyoendelea.

Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika vituo vya Kuandikishia na kuboresha taarifa za Wapiga Kura.
Post a Comment