" DENI LA SERIKALI LAPANDA KUTOKA TRILIONI 82.25 HADI TRILIONI 97.35

DENI LA SERIKALI LAPANDA KUTOKA TRILIONI 82.25 HADI TRILIONI 97.35

  Na. MWANDISHI WETU

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Dkt. Charles Kichere, leo March 27,2025 amewasilisha ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo amesema deni la Serikali limeongezeka na kufikia Tsh.trilioni 97.35 kutoka Tsh. trilioni 82.25 katika mwaka wa fedha uliopita.


Dkt . Kichere amesema “Kufikia June 30,2024 deni la Serikali lilifikia Tsh. trilioni 97.35, kiasi hiki kimeongezeka kutoka Tsh. trilioni 82.25 kilichokuwa kimeripotiwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 hii ni sawa na ongezeko la Tsh. trilioni 15.1 ambalo ni sawa na asilimia 18.36”

“Deni hilo linajumuisha deni la ndani la Tsh. trilioni 31.95 na deni la nje la Tsh. trilioni 65.40, tathmini ya uendelevu wa deni la Serikali imebaini kuwa deni la Taifa bado ni himilivu”

Post a Comment

Previous Post Next Post