Na Mapuli Kitina Misalaba
Muasisi wa Moyo wa Mwanamke Shujaa Organization, Dr. Magdalena Kongera, ambaye pia ni sehemu ya Kamati Tendaji na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM, amewaasa wanawake katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kuungana katika kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, unyanyasaji wa kijinsia, ndoa za utotoni, mimba za ujiraoni kwa mabinti, na vitendo vya ushoga na usagaji.
Dr. Kongera amesisitiza umuhimu wa kushirikiana katika kuzuia vitendo vya kikatili na vile vinavyosababisha madhara kwa watoto na jamii, akisema kuwa ni lazima wanawake na vijana waungane ili kukomesha maovu haya.
Ameongeza kuwa, ni muhimu kupinga ndoa za jinsia moja na kuendeleza utamaduni wa kupinga utelekezwaji wa watoto, ambao unachochea madhara makubwa kama vile kubakwa na kupata maambukizi ya HIV.
Mwisho, Dr. Kongera amewaomba wanawake wote, mabinti na wavulana kuungana na taasisi yake katika kupigania haki na ustawi wa wanawake na watoto.
Ameahidi kuendelea na kazi hiyo kwa ujasiri mkubwa na amewasihi wanawake na mabinti wote kumchagua Samia Suluhu Hassan kwa kura nyingi za ndiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Post a Comment