Kamati ya kudumu ya Bunge ya TAMISEMI imeridhishwa na ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika hospitali ya Halmashauri ya manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, linalojengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 6.7 fedha za mapato ya ndani.
Akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua ujenzi wa jengo hilo, mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba, amesema jengo hilo ni mkombozi kwa akina mama wanaofika kujifungua kwenye hospitali hiyo.
“Leo ninaonyesha furaha kubwa kwa niaba ya wanawake wa Kahama, tuliopata Bahati ya kujifungulia kwenye hospitali hii ya manispaa ya Kahama, na mimi ni mmoja wao, na likikamilika hili jengotutaweza kujifungua kwenye mazingira yenye staha, yakutustiri sisi wanawake na uanauke wetu” Amesema Makamba
Mbunge wa jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba amesema idadi hiyo ni ile ya wanawake wanafika hospitali, lakini jamii bado wapo wanaojifungulia nyumbani na baadae kufikishwa hospitali, hivyo idadi ya wanaozaliwa kwa mwezi ni karibu 1000 kwa mwezi.
Amesema idadi ya watu inaongezeka kila siku kutokana Kahama kupakana nan chi jirani lakini pia kuwa na migodi midogo mingi, hivyo akaiomba serikali kuongeza bajeti kwa hospiatali hiyo, ili kuwahudumia vyema wateja ambao wengi wanakimbilia katika hospitali hiyo.
Naibu Waziri ofisi ya Rais Tamisemi Zainab Katimba amesema serikali itaongeza nguvu kwenye jengo la mama na mtoto Kahama ili likamilike haraka na kuanza kutoa huduma.
“Halmashauri wana wajibu wa kuanza ujenzi wa miradi hii mbalimbali ya maendeleo, lakini sisi kama serikali kuu tunakuja kuongeza nguvu ili kuhakikisha jengo hili linakamilika” Amesema Katimba
Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo, Meneja wa mradi wa Manispaa ya Kahama, Mashala Mboje amesema, ujenzi wake ulianza julai 15 mwaka 2022 na unatarajia kukamilka julai mwaka huu 2025, na linajengwa na Mkandarasi Suma JKT ya Geita kwa gharama ya Sh 6.7 Bilioni fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.
Kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Kahama Dk Baraka Msumi amesema kukamilika kwa jengo hilo ni mkombozi kwenye huduma za mama na mtoto hospitalini hapo kwani litaondoa msongamano mkubwa uliopo sasa.
MWISHO.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba
Post a Comment