
Na Halima Issa Hassani, Misalaba Media
Rai imetolewa kwa Wakazi wa Dodoma kuendelea
kuhamasisha jamii kuhusu zoezi la kupanda miti
ili kusaidia utunzaji wa Mazingira na kuendelea kupambana na mabadiliko
ya Tabianchi, kwani mbinu ya kukabiliana na hali hiyo ni kupanda miti kwa
wingi.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala msaidizi Sekta
za Uchuni na Uzalishaji Mkoa wa Dodoma Bi.Aziza Mumba Machi, 2025 Jijini Dodoma
mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upandaji miti ya Kampeni inayosema Mti
wangu,Birthday yangu inayoratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma katika
eneo la wazi la ukanda wa kijani, Nanenane kata ya Nzuguni.
Aidha Bi. Aziza ameongeza kuwa tangu walipoanza
kampeni hii ya Mti wangu,Birthday yangu wamekwisha kupanda miti takribani
Milioni 4 na laki 8 na sio kupanda tu bali hata katika kuendelea kuitunza ili
watu wajue kuwa mti ukiutunza unakua vizuri.
Kampeni hii ya mti wangu,Birthday yangu imeasisiwa
na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bwana Gaspar Mmuya kwa kupanda miti kwenye
siku za kuzaliwa ambayo hufanywa kila tarehe 18 ya mwezi.
Post a Comment