" MATAMANIO YETU NI KUONA NINAYE MUONGOZA ANAFANIKIWA

MATAMANIO YETU NI KUONA NINAYE MUONGOZA ANAFANIKIWA


WANAWAKE wafanyakazi walio idara za serikali wamesema nafasi zao za utumishi kwenye jamii zinapashwa kuakisi uwajibikaji vilevile maadili mema Ili kuwezesha wananchi kuwa na imani nao katika nafasi wanazosimamia.

Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti Jijini Mwanza na wadau hao walipokuwa wakizungumza na Vyombo vya Habari kufuatia maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo yamehitimishwa hivi karibuni kitaifa Mkoani Arusha.

Afisa Elimu wa Kata ya Pamba Edna Kajungu alisema wanawake ni watumishi wanaojituma katika mambo yao ya kila siku wayafanyayo hivyo yeye hufurahia mafanikio wayapatayo watu anaowaongoza.

Alisema kufanikiwa kwa mtu aliye chini yake ni faraja kwake kwani hali hiyo humuwezesha kuona kuwa jambo analosimamia linaeleweka vizuri kwenye jamii.

Kajungu alisema uongozi wa mwanamke ni wa kipekee akimtaja Rais Samia Suluhu Hassan alivyoweza kusimamia kwa ukaribu miradi ya maendeleo ambayo imeleta tuja kwa Taifa.



Post a Comment

Previous Post Next Post