" MBABE WA ALI BONGO ATIA NIA YA URAIS.

MBABE WA ALI BONGO ATIA NIA YA URAIS.


Na Belnardo Costantine, Misalaba Media 
Kiongozi wa kijeshi na Rais wa mpito wa Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema, ambaye aliongoza mapinduzi ya 2023 ili kumaliza miaka 55 ya utawala wa Omar Bongo, alitangaza Jumatatu kuwa atawania urais mwezi Aprili.

Oligui alikuwa ameahidi kurudisha mamlaka kwa raia katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la katikati mwa Afrika kwa muda mfupi baada ya kuondolewa madarakani kwa rais Ali Bongo Ondimba Agosti 2023.


Post a Comment

Previous Post Next Post