" MCHUNGAJI ATUPWA JELA KOSA LA UVAMIZI WA ENEO

MCHUNGAJI ATUPWA JELA KOSA LA UVAMIZI WA ENEO

 

Na Belnardo Costantine, Misalaba Media

Mchungaji wa Mitume na Manabii Daudi Mashimo inamehukumiwa kifungo cha miaka miwili na miezi sita Jela na Mahakama ya Wilaya Kinondoni baada ya kukutwa na hatia ya jinai ya kuvamia eneo la watu.

Mchungaji Mashimo alikuwa akikabiliwa na mashtaka kadhaa ya kuvamia na kuishi kwenye eneo la mlalamikaji Flora Jonasi, kuharibu mali kwa makusudi, na kufanya vurugu dhidi ya Ramsoni.

Mahakama ilimkuta na hatia katika mashtaka ya mawili, huku ikimuondolea shtaka  moja ambalo wamemkuta hana hatia.

Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mtuhumiwa ameshauri ndugu, jamaa na marafiki kukata rufaa ikiwa hawajaridhika na uamuzi huo

Post a Comment

Previous Post Next Post