" MDEE AWATAKA WATUMISH WA UMMA KUTOA HUDUMA STAHIKI

MDEE AWATAKA WATUMISH WA UMMA KUTOA HUDUMA STAHIKI

 
Na Belnardo Costantine, Misalaba Media 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Mbuge kutoka "CHADEMA " Mhe. Halima Mdee, amewataka Watumishi wa Umma na Viongozi kutekeleza wajibu wao kwa ufasaha ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Mdee akizungumza katika ziara ya Kamati hiyo kukagua miradi mbalimbali ya afya na elimu inayotekelezwa Halmashauri ya Kyela, mkoani Mbeya, amesema 
"Kila mmoja atekeleze wajibu wake kwa wakati na kwa ufasaha, viongozi hawatakuwa na haja ya kuja kukagua." 

Ameeleza kuwa kutokana na ukubwa wa nchi, haiwezekani kwa kiongozi mmoja kutembelea kila mahali kutoa huduma, hivyo majukumu hayo yamekabidhiwa kwa Watumishi wa Umma ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki.

Aidha, amewataka Watumishi wa Umma kutekeleza maelekezo yanayotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge na kuhakikisha wanazitatua dosari zinazobainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kutoa taarifa sahihi.

Sambamba na hayo Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais "TAMISEMI," Mhe. Dkt. Festo Dugange, amesema Ofisi yake imechukua maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati na itayasimamia kikamilifu katika utekelezaji wake.

Hatahivyo Mhe. Dkt. Dugange amewataka Watumishi wa Umma kuhakikisha fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zinatumika ipasavyo ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kuzingatia thamani ya fedha.






Post a Comment

Previous Post Next Post