Na:Mwandishi wetu SHINYANGA
Katika Kuhakikisha jamii inaondokana na umasikini na
kujikwamua kiuchumi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imetoa mafunzo kwa
jumla ya vikundi (19) vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, vikundi
vilivyokidhi kupata mkopo wa asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri kupitia
mapato ya ndani mikopo isiyo na riba.
Akizungumza leo Machi, 22,2025 Katika Mafunzo haya Afisa
maendeleo ya jamii kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Nyanjula
Kiyenze amesema jumla ya Tsh. Milion 225,879,500/= zimetengwa kwa ajili ya vikundi hivyo ambapo Kwa mujibu wa
Sheria ya mwaka 2024 inatutaka kabla ya vikundi vilivyokidhi kupata mkopo
havijapokea ni lazima vipate mafunzo ili kuongeza uelewa juu ya mkopo huo.
"jumla ya Tsh milion
225,879,500/= ambapo vikundi vya wanawake ni Tsh 127,927,500/= vikundi
vya vijana Milion 123,952,000/= na Mtu mwenye ulemavu ni Tsh4,000,000/=
zimetolewa na Halmashauri mikopo ya asilimia kumi isiyokuwa na riba ili vikundi hivi viweze kujikwamua
kiuchumi". Amesema Bi. Nyanjula.
Awali akifungua mafunzo haya Mstahiki Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko amevisisitiza vikundi hivyo kuwa na
nidhamu ya Fedha, kuwa waaminifu Katika kurejesha mikopo hiyo ili iweze
kuwanufaisha wananchi wengine.
"Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais wetu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inafanya kila liwezekanalo
Kuhakikisha makundi haya yanajikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini,
Fedha hizi ni mapato ya ndani ambayo ni Kodi za wananchi, sasa niombe kuwa na
nidhamu ya Fedha hizi, kuweni waaminifu Katika kurejeshe ili vikundi vingine
navyo vipate kama ninyi mlivyopata. Amesema". Mhe Masumbuko
Katika vikundi hivyo jumla ya mada (5) zimefundishwa
Usimamizi wa vikundi, Utatuzi wa migogoro, Usimamizi wa biashara, Utunzaji wa
kumbukumbu pamoja na Msaada wa kisheria
(MSLAC) zimefundishwa kwa vikundi 19 kutoka kata 9 kati ya Kata 17 za
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga zilizokidhi kupata mkopo huo.

Msitahiki meya wa Halmashauri ya manispaa ya shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akifungua mafunzo kwa vikundi vilivyokidhi kupata mkopo wa asilimia kumi (4:4:2) kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu
Afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya manispaa ya shinyanga Bi. Nyanjula Kisenye akitoa mafunzo ya mikopo ya asilimia kumi kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. vilivyokidhi kipewa mkopo huo.
Afisa kutoka kitengo cha msaada wa kisheria (Mama Samia legal Aid Campaign) Halmashauri ya manispaa ya shinyanga Bi. Omana Joseph akitoa mafunzo ya msaada wa kisheria katika mafunzo hayo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
vikundi vilivyokidhi kupata mkopo wa asilimia kumi vikisikiliza mafunzo inayotolewa na halmashauri bila riba
vikundi vilivyokidhi kupata mkopo wa asilimia kumi vikisikiliza mafunzo inayotolewa na halmashauri bila riba
Afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya manispaa ya shinyanga Bi.Wema Mashaka ambaye pia ni afisa malalamiko akitoa mafunzo juu ya maada ya migogoro kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. vilivyokidhi kupewa mkopo huo.
Post a Comment