
Na Mapuli Kitina
Misalaba
Mkutano wa MISA-TAN na wadau (MISA-TAN - Wadau
Summit 2025) unaotarajiwa kufanyika Machi 14, 2025, jijini Dodoma, umeendelea
kupata msukumo baada ya taasisi mbalimbali kuthibitisha kushiriki kama
wafadhili wa kongamano hilo.
Mkutano huo unaoandaliwa
na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN),
utawakutanisha waandishi wa habari na wadau wa sekta ya habari na mawasiliano
ili kujadili masuala muhimu yanayohusu uhuru wa vyombo vya habari, maendeleo ya
sekta hiyo, na ushirikiano baina ya wadau.
Miongoni mwa taasisi
zilizojitokeza kufadhili mkutano huo ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Bima
ya Afya (NHIF), Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Mamlaka ya Udhibiti wa
Mawasiliano Tanzania (TCRA), na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(PCCB).
Taasisi nyingine ni
Shirika la TASHICO, Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC), na
Pan-African Constructive Journalism Initiative (PACJI). Ushiriki wa taasisi
hizo unatarajiwa kuleta mchango mkubwa katika kufanikisha kongamano hilo na
kujenga mazingira bora ya tasnia ya habari nchini.
Mkutano huo utakuwa na
mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule.

Post a Comment