" MWEZI UMEANDAMA! JUMATATU NI SIKU YA EID!

MWEZI UMEANDAMA! JUMATATU NI SIKU YA EID!

MWEZI UMEANDAMA, WATANZANIA KUADHIMISHA EID AL-FITR JUMATATU

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza kuwa mwezi umeandama rasmi tarehe 30 Machi 2025, hivyo Waislamu nchini wataadhimisha Sikukuu ya Eid Al-Fitr siku ya Jumatatu, tarehe 31 Machi 2025.

Tangazo hilo limetolewa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir Ali Mbwana, kupitia msemaji wake, Dr. Harith Nkussa.

Sikukuu ya Eid Al-Fitr huadhimishwa na Waislamu kote duniani kama ishara ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambapo waumini hujumuika kwa ibada na kusherehekea kwa furaha.

Eid Mubarak kwa Waislamu wote!

Post a Comment

Previous Post Next Post