" NAFASI YA MWANAMKE KATIKA JAMII NA HARA kati ZA USAWA WA KIJINSIA

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA JAMII NA HARA kati ZA USAWA WA KIJINSIA


"Mwanamke katika jamii mbali mbali huwa ana nafasi yake maalumu, na nafasi yake huwa inaendana na namna ya jamii yake inavyompa thamani kiumbe huyu. Kila jamii hua inamuhesabu mwanamke kuwa ni mmoja kati ya viungo vya jamii, lakini tofauti huwa inapatikana kwa namna ya kila jamii inavyo muangalia mwanamke huyo.

Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka. Siku hiyo ilianza kuadhimishwa tarehe 8 Machi 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kuridhia siku hii kutumika kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake.

Siku hii pia huongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume katika jamii.

Tunapoelekea katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, naomba niwakumbushe jambo moja Wanawake wenzangu.

Mapambano yetu ni katika hali ya kuleta urahisi na usawa wa upatikanaji wa rasilimali na fursa bila kujali jinsia, ikiwa ni pamoja na ushiriki wa kiuchumi, maamuzi na jitihada za kuleta usawa kati ya jinsia zote mbili na kuondokana na dhuluma mbalimbali za jinsia moja dhidi ya nyingine zilizotawala historia ya binadamu.

Hivyo Wanawake hatupambani na Wanaume kama wengi wanavyofikiria, bali tunapambana na mifumo kandamizi dhidi yetu, hatuhitaji kubebwa kwenye kupata Fursa mbalimbali bali tupewe Fursa ikiwa tunakidhi vigezo stahiki, na bila shaka niwaombe Wanawake tuendelee kuwa watiifu kwa wanaume zetu, tunawahitaji sana kwenye Mapambano haya kama vile wao wanavyotuhitaji kwenye safari za mafanikio.."

              Cde. Jamillah Miyonga
              _M/kiti UWT (W) Kilosa

#Tukajiandikishe..


Post a Comment

Previous Post Next Post