HomeKIMATAIFA RAIS SAMIA ASHUHUDIA HISTORIA MPYA NAMIBIA, AMUUNGA MKONO RAIS NANDI-NDAITWAH Misalaba March 21, 2025 0 Na Halima Issa, Misalaba MediaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameungana na viongozi mbalimbali duniani kushuhudia na kusherehekea historia mpya nchini Namibia kwa kuapishwa kwa Rais wa kwanza mwanamke wa taifa hilo.Hafla hiyo imefanyika Machi 21, 2025, katika Ikulu ya Windhoek, ambapo Rais Samia amempongeza Rais huyo Nandi-Ndaitwah kwa ushindi wake na kuonyesha mshikamano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Namibia.Nandi - Ndaitwah ameandika historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuongoza taifa hilo, hatua inayotajwa kuwa muhimu katika kusukuma mbele usawa wa kijinsia na uongozi wa wanawake barani Afrika. You Might Like View all
Post a Comment