Na Halima Issa, Misalaba Media
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Machi 22, 2025, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji, Rais Samia alisema kuwa lengo la gridi hiyo ni kuwezesha upatikanaji wa maji katika maeneo yote ya nchi. Kwa mfumo huu, maji yatakayokusanywa yataweza kusambazwa kwa ufanisi hata pale ambapo eneo moja litakumbwa na ukame, hivyo kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji bila changamoto kubwa.
"Hii gridi ya maji itasaidia kuweka usawa katika mgao wa maji na kuhakikisha hakuna eneo linalokosa huduma kwa sababu ya ukame au changamoto nyingine za mazingira," alisema Rais Samia.
Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wote, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha sekta ya maji nchini.
Post a Comment