Na Belnardo Costantine, Misalaba Media
Serikali na familia ya Margaret Nduta, mwanamke wa Kenya aliyehukumiwa kifo nchini Vietnam baada ya kunaswa na dawa za kulevya, bado wanasubiri mawasiliano kuhusu hatima yake.
Waziri wa Mambo ya Kigeni Musalia Mudavadi kwa mara ya kwanza alizungumzia sakata la Nduta akiwahakikishia Wakenya kwamba wanafanya kila juhudi kuzuia kunyongwa kwake kwa kudungwa sindano, kulingana na runinga ya Citizen TV nchini Kenya.
Mudavadi ameongeza kuwa ofisi yake inazo taarifa za Wakenya wapatao 1,000 katika mataifa ya nje ambao wanakabiliwa na adhabu ya kifungo jela au wamefungwa kwa makosa tofauti.
Serikali imewasihi Wakenya wanaosafiri ng’ambo kuwa waangalifu na kuepuka kutumbukia katika mitego ya kubeba mizigo ya watu bila kujua nini walichobeba.
Post a Comment