WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea,Watendaji Wakuu wa Wakala wa Serikali,Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma,Wakurugenzi wa Majiji,Manispaa na Miji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya kilichofanyika Machi 3,2025 jijini Dodoma.
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu ,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea,Watendaji Wakuu wa Wakala wa Serikali,Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma,Wakurugenzi wa Majiji,Manispaa na Miji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya kilichofanyika Machi 3,2025 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene (hayupo pichani), wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea,Watendaji Wakuu wa Wakala wa Serikali,Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma,Wakurugenzi wa Majiji,Manispaa na Miji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya kilichofanyika Machi 3,2025 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene (hayupo pichani), wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea,Watendaji Wakuu wa Wakala wa Serikali,Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma,Wakurugenzi wa Majiji,Manispaa na Miji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya kilichofanyika Machi 3,2025 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene (hayupo pichani), wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea,Watendaji Wakuu wa Wakala wa Serikali,Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma,Wakurugenzi wa Majiji,Manispaa na Miji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya kilichofanyika Machi 3,2025 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea,Watendaji Wakuu wa Wakala wa Serikali,Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma,Wakurugenzi wa Majiji,Manispaa na Miji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya kilichofanyika Machi 3,2025 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene,amesema Serikali imeendelea kuboresha mifumo ya kiutawala na usimamizi wa Rasilimaliwatu ya kidijitali ili kurahisisha utendaji kazi na kuboresha utoaji wa huduma katika Utumishi wa Umma.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo Machi 3,2025 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea,Watendaji Wakuu wa Wakala wa Serikali,Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma,Wakurugenzi wa Majiji,Manispaa na Miji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya.
Amesema Mifumo hiyo inajumuisha Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara, Mfumo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma (ess) wenye madirisha ya e- Utendaji Kazi, e-Uhamisho, e-Mikopo, e-Likizo na e- Salary slip; Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji ya Watumishi (HR Assesment); Masjala Mtandao (e-office); Mfumo wa barua pepe wa Serikali (GMS); e-vibali mbadala; Mfumo wa Ajira (Ajira Portal) na Mfumo wa Ushughulikiaji wa Mrejesho wa Wananchi (e-Mrejesho).
“Mifumo hiyo inaendelea kuleta mageuzi ya kiutendaji na utoaji wa huduma wenye lengo la kumfikia na kumhudumia mwananchi kwa haraka, gharama nafuu na kwa ufanisi wa hali ya juu. Mkiwa viongozi mnatarajiwa kuwa vinara katika kuhimiza matumizi ya mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali.”amesema Mhe.Simbachawene
Aidha amesema Mifumo hiyo imeendelea kusaidia kutatua kero za Watumishi wa Umma na Wananchi kwa kuongeza uwazi na uwajibikaji wa Watendaji kwa wapokea huduma.
Amesema kuwa baadhi ya kero zilizotatuliwa kupitia Mifumo hiyo ni pamoja na kuwezesha Mamlaka za juu za nchi kufahamu hali ya utendaji kazi wa watumishi wa Umma na kuchukua hatua stahiki; kubaini mahitaji halisi ya watumishi katika Utumishi wa Umma; kushughulikia hamisho za watumishi kwa wakati na kudhibiti udanganyifu katika michakato ya uhamisho na ajira.
Ametaja kero nyingine zilizotatuliwa ni kufanya msawazo wa watumishi ndani na nje ya taasisi;, kuboresha ufanisi wa utendaji kazi na kuwezesha wapokea huduma kufuatilia utatuzi wa malalamiko kimtandao badala ya kusafiri umbali mrefu kwenda katika Vituo vinavyotoa huduma hivyo kupunguza gharama za watumishi wa Umma na wananchi katika kufuatilia hoja mbalimbali katika Ofisi za Umma.
Hata hivyo amesema kuwa ndoa nyingi za watumishi wa umma zinakufa kutokana na wenza kukaa mbalimbali na kwamba wiki ijayo vitatolewa vibali zaidi ya 200 ili wasogezwe na familia zao.
Pia amesema kuwa Jumatatu ya wiki ijayo (Machi,10, 2025) Mawaziri watatu watakutana na Umoja wa Walimu wasio na ajira Tanzania (NETO) kwa ajili kujadiliana nao.
Naye, Naibu Waziri, Ofisi hiyo, Deus Sangu, amesema amejaribu kufuatilia na kubaini baadhi ya malalamiko ni uzembe na wengine kudai limekwama Utumishi au TAMISEMI jambo ambalo si kweli.
Alieleza kuwa mamlaka za ajira zina malimbikizo ya mishahara na sehemu kubwa baadhi wametumia kama ni sehemu ya biashara kwamba mtumishi ambaye hatoi chochote jambo lake halishughulikiwi.
Pia, alisema baadhi ya waajiri kutowapa mafunzo elekezi watumishi wapya jambo ambalo linahatarisha utumishi wa umma na inasababisha wingi wa mashauri ya kinidhamu.
Awali, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Juma Mkomi, amesema kuwa kupitia tathmini mbalimbali inaonesha bado kuna changamoto mbalimbali za kiutendaji katika masuala ya utawala na usimamizi wa rasilimali watu katika utumishi wa umma kutokana na kutozingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo.
“Hali hii imesababisha kushuka kwa hali ya utendaji kazi kwa watumishi na hivyo kuchelewesha utoaji huduma kwa wananchi au kutoa huduma kwa viwango visivyoridhisha,”amesema
Post a Comment