Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndg. Stephen Masato Wasira, anatarajiwa kuanza ziara yake mkoani Shinyanga kesho, Machi 26, 2025.
Kwa mujibu wa katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Shinyanga Richard Raphael Masele, ziara hiyo inalenga kuimarisha chama, kusikiliza changamoto za wananchi, na kueleza mwelekeo wa CCM katika maendeleo ya taifa.
Katika ratiba yake, Wasira ataanzia Shinyanga Mjini Machi 26, kisha ataelekea Kahama Mjini Machi 27, ambako atafanya mkutano wa hadhara, na kumaliza ziara yake Machi 28 katika eneo la Maganzo, wilayani Kishapu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment