Mhandisi Yahya Samamba ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Madini amesema Serikali imetoa fedha nyingi na kujenga Kituo kikubwa cha Jemolojia ili kuwa na kituo bora,chenye mashine bora na Wataalam bora nchi nzima ili kuhakikisha Madini hasa ya vito yanaongezewa thamani hapa nchini katika viwango vinavyohitajika kabla ya kusafirisha kwenda nje ya Nchi
Mhandisi Samamba ameyaeleza hayo Machi 26, 2025 Jijini Dodoma katika hafla fupi ya utiaji saini wa makubaliano kati ya Kampuni Sun Set kutoka Tailand na Kituo cha Jemolojia Tanzania iliyoko chini ya Wizara ya Madini.
Na kuahidi kuwa watasimamia utaratibu na namna ambavyo makubaliano hayo yatatekelezwa ili pande zote mbili waweze kunufaika na makubaliano hayo.
"Kupitia Kituo chetu chetu cha TGC Mhe Rais ameweka fedha nyingi,tumejenga jengo kubwa kabisa ambacho ni kituo kikubwa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla ambapo lengo ni kuhakikisha tunakuwa na kituo bora,chenye mashine bora,chenye wanafunzi bora na Wataalam bora ili waweze kuenea nchin nzima kuhakikisha kwamba Madini hasa ya vito yanayotokea nchini yanaongezewa thamani hapa nchini mpaka viwango vinavyohitajika na ndipo yaweze kusafirishwa kwenda nje ua Nchi".
Pia amebainisha lengo la kusaini mkataba huo ambapo amesema kuwa makubaliano haya ni moja ya utekelezaji wa Sera ya madini ya mwaka 2009 ambayo inataka Madini yote yanayochimbwa ndani ya nchi ya aina zote yanaongezewa tahamani ndani ya nchi kabla ya kwenda nje.
Kwa upande wake Mratibu wa Kituo cha Jemolojia Tanzania(TGC) Mhandisi Ally Noganga amesema kuwa dhumuni la Serikali kuingia makubaliano na Kampuni ya Sun Set ni kuboresha taaluma ya masuala mazima ya Jemolojia kwa maana ya Sayansi ya Madini ya vito pia kuongeza ubunifu katika suala zima la ukataji na ung'arishaji wa madini ya vito.
Post a Comment