Na Belnardo Costantine, Misalaba Media
wa mara ya kwanza katika kipindi cha mwaka mmoja, marais wa DRC , Félix Tshisekedi, na Rwanda Paul Kagame, wamefanya mazungumzo.
Mkutano huo wa ana kwa ana ulifanyika Jumanne, Machi 18, nchini qatar, chini ya upatanishi wa Emir, katika jaribio la kutafuta suluhu la mzozo wa usalama mashariki mwa DRC.
Kinshasa inashutumu jirani yake kwa kuunga mkono uasi wa M23, ambao umeteka sehemu kubwa ya majimbo ya Kivu Kusini na Kaskazini. Shutuma zinazoungwa mkono na ripoti kadhaa za Umoja wa Mataifa, lakini zimekanushwa na Kigali .
Wawili hao wameafikia makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano Mashariki ya DRC.
Post a Comment