" UKRAINE NA MAREKANI KUKUTANA LEO SAUDI ARABIA

UKRAINE NA MAREKANI KUKUTANA LEO SAUDI ARABIA


Na Belnardo Costantine, Misalaba Media
 
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy y
Amewasi nchini saudi Arabia kuhudhuria mazungumzo yatakayofanyika leo kati ya nchi yake na Marekani kutafuta namna ya kumaliza vita dhidi ya ukraine.

Rais Zelensky aliwasili jijini Jedda siku ya Jumatatu na kupokea kijeshi sambamba  nakupigiwa gwaride la mapokezi ya heshima.

Baada ya kuwasili walifanya mazungumzo ya amani na mwana Mfalme Mohammed bin Salman, kuelekea mazungumzo hayo kati ya nchi yake na Marekani.

Kiongozi huyo wa Ukraine, anatarajiwa kuwasilisha kwa Marekani, mpango wa kusitisha vita kwa kiwango fulani dhidi ya Urusi, akitumai kupata uungwaji mkono kutoka kwa rais Donald Trump.


 

🍺 LADHA HALISI, BURUDANI ISIYO NA MFANO

Post a Comment

Previous Post Next Post