" UMOJA WA MACHIFU TANZANIA WAUNGANA NA WANAWAKE KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

UMOJA WA MACHIFU TANZANIA WAUNGANA NA WANAWAKE KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


 Na Mapuli Kitina Misalaba 

Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) umeungana na wanawake wote nchini kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.

Kupitia Mwenyekiti wake, Chifu Antonia Tonisiza Sangalali, UMT umeeleza dhamira yake ya kuendelea kuwaunga mkono wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo. 

Katika salamu zake za pongezi, Umoja huo umemwakilisha Mkuu wa Machifu Tanzania, Chifu Hangaya, akimtambua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kama kiongozi mwanamke anayetoa mfano wa kuigwa kwa wanawake wote nchini.

UMT imeeleza kuwa mchango wa wanawake katika jamii hauwezi kupuuzwa, kwani wao ni nguzo muhimu katika maendeleo ya taifa. 

Aidha, Umoja huo umetoa wito kwa jamii yote kushirikiana katika kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi sawa katika kila sekta.

Siku ya Wanawake Duniani ni maadhimisho yanayotumika kuhamasisha usawa wa kijinsia, kuenzi mafanikio ya wanawake na kushinikiza hatua zaidi katika kuwawezesha wanawake duniani kote.

Safari ya Ladha: Ubora wa East African Spirits (T) Ltd

Post a Comment

Previous Post Next Post