" UMOJA WA WANAUME TANZANIA WATAKIWA KUSHUGHULIKIA MMOMONYOKO WA MAADILI KATIKA JAMII

UMOJA WA WANAUME TANZANIA WATAKIWA KUSHUGHULIKIA MMOMONYOKO WA MAADILI KATIKA JAMII


Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini, Mhe. Godwin Gondwe, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa ufunguzi wa kikao cha viongozi wa Umoja wa Wanaume Tanzania kilichofanyika mjini Singida, leo Machi 22, 2025.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Umoja wa Wanaume Tanzania wamesisitizwa kuchukua hatua madhubuti kushughulikia mmomonyoko wa maadili katika familia na jamii kwa ujumla, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza au kumaliza kabisa vitendo vibaya kama ulawiti, ubakaji, ushoga, na tabia zisizofaa kwa maadili ya Kitanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini, Mhe. Godwin Gondwe, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa ufunguzi wa kikao cha viongozi wa Umoja wa Wanaume Tanzania kilichofanyika mjini Singida, amesisitiza umuhimu wa umoja huo katika kuimarisha maadili.

Mkuu wa Mkoa amefurahishwa sana na kuanzishwa kwa umoja huu, ambapo amenituma kuwaambie jambo la kwanza ni kuhakikisha mnashughulikia suala la maadili katika jamii. Muendelee kulizungumzia kwa lugha fasaha ili ujumbe uwafikie wanajamii kwa urahisi, amesema Gondwe.

“sauti ya mwanaume inahitajika katika jamii kuanzia ndani ya familia kama zilivyo sauti za watu wengine. Wapo wazazi wenye tabia za kuwalawiti watoto wao. Kesi kama hizo zipo kwenye ofisi yangu, hivyo Umoja huu una kazi ya kuhakikisha maadili yanadumishwa katika jamii, ameeleza DC Gondwe.

Viongozi wa Umoja wa Wanaume Tanzania pia wametakiwa kushirikiana na viongozi wa dini ili kuimarisha maadili na kuhakikisha kila mtu anatambua wajibu wake ndani ya familia na jamii kwa ujumla. Wanaume wanapaswa kuwa wabunifu na wachapa kazi badala ya kuwa tegemezi katika maisha yao, ameongeza Gondwe.

Katibu Mkuu wa Umoja huo, John Sagata, akiwasilisha taarifa ya umoja, amesema kuwa lengo kuu ni kuwatambua wanaume, kuwaelimisha, na kuwaunganisha na taasisi mbalimbali za serikali zinazotoa huduma muhimu, ikiwemo afya.

Tunatarajia kuwawezesha wanaume kuwa na jukwaa maalum la kujadili changamoto zao, kama vile maradhi ya tezi dume, shinikizo la damu, na kisukari, pamoja na masuala yanayohusiana na hali ya maisha yao katika jamii, amesema Sagata.

Aidha, umoja huo utahakikisha kuwa wanaume wanatimiza wajibu wao katika familia na jamii, wanapata haki zao za msingi, na wanashiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Umoja huo pia umeahidi kufuatilia na kuhakikisha wanaume hawafanyiwi ukatili na makundi mengine, ikiwemo wenza wao, watoto, na jamii kwa ujumla.

Mojawapo ya malengo ni kuhakikisha wanaume wanafikiwa na fursa muhimu zinazotolewa na serikali, ikiwa ni pamoja na mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi, ameeleza Sagata.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanaume Tanzania, Claude Kimu, amesema kuwa taasisi hiyo ni mpya na imepata usajili wake hivi karibuni kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Malengo yetu ni kuhakikisha wanaume wanarudi kwenye majukumu yao ya msingi ambayo walipewa na Mwenyezi Mungu kama nguzo ya familia, jamii, na taifa kwa ujumla, amesema Kimu.

Amesema kuwa serikali inapaswa kuwatambua wanaume kama kundi muhimu na kuwahudumia kwa namna sawa na makundi mengine kama vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu.

Tunahitaji kuona wanaume wakihusishwa katika mipango ya maendeleo, hususan kupitia mikopo isiyo na riba kubwa, ili waweze kujihusisha na miradi ya kiuchumi na kujitegemea, amesisitiza Kimu.

Aidha, ameeleza kuwa baadhi ya watoto wa kiume wanashiriki katika vitendo visivyo vya kimaadili, ikiwemo ushoga, ulawiti, na matumizi ya dawa za kulevya, na kwamba umoja huo utahakikisha kuwa elimu sahihi inatolewa kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu ili kuzuia mmomonyoko wa maadili.

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Arusha, Tabora, na Manyara, pamoja na viongozi wa dini kutoka Mkoa wa Singida.

Umoja wa Wanaume Tanzania umetangaza kuwa kaulimbiu yake ni “WANAUME – NGUZO YA JAMII” na umejipanga kuhakikisha jamii inaishi kwa misingi ya maadili, upendo, na mshikamano.


Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini, Mhe. Godwin Gondwe, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa ufunguzi wa kikao cha viongozi wa Umoja wa Wanaume Tanzania kilichofanyika mjini Singida, leo Machi 22, 2025.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini, Mhe. Godwin Gondwe, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa ufunguzi wa kikao cha viongozi wa Umoja wa Wanaume Tanzania kilichofanyika mjini Singida, leo Machi 22, 2025.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanaume Tanzania Claude Kimu, akizungumza kwenye kikao hicho leo Machi 22, 2025.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanaume Tanzania Claude Kimu, akizungumza kwenye kikao hicho leo Machi 22, 2025.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanaume Tanzania John Sagata, akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi katika kikao hicho leo Machi 22, 2025.

Viongozi mbalimbali



Post a Comment

Previous Post Next Post