Na Halima Issa, Misalaba Media
Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki (COSOTA) Bi.Doreen Sinare amesema Usajili wa kazi zinazolindwa na Sheria ya hakimiliki na hakishiriki umeongezeka kwa asilimia 70 ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Ambapo mpaka Februari 2025 COSOTA imesajili kazi za Sanaa na uandishi 11,519 na Wabunifu 3,436 ambapo idadi hii imetokana na utoaji wa elimu na mafunzo ya hakimiliki.
Bi. Sinare ameeleza hayo leo hii Jijini Dodoma Machi 21,2025 Katika Mkutano wake na Wanahabari akielezea mafanikio na mwelekeo wa Taasisi hiyo katika miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.
"Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, usajili wa kazi zinazolindwa na Sheria ya hakimiliki na hakishiriki umeongezeka kwa asilimia 70 Ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kuanzia mwaka 2021 mpaka Februari 2025, COSOTA, imesajili kazi za Sanaa na uandishi 11,519 na Wabunifu 3,436".
Post a Comment