" WAISLAMU SHINYANGA WATAKIWA KUENDELEA KUSHIKILIA MISINGI YA DINI BAADA YA RAMADHANI

WAISLAMU SHINYANGA WATAKIWA KUENDELEA KUSHIKILIA MISINGI YA DINI BAADA YA RAMADHANI


Na Mapuli Kitina Misalaba

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kuzingatia misingi ya dini kwa kutenda mambo mema kama walivyofanya katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Sheikh Makusanya ametoa wito huo leo baada ya Eid - alfitr iliyofanyika katika Uwanja wa Sabasaba Kambarage, Mjini Shinyanga.

Ametoa rai kwa waumini kusherehekea Sikukuu ya Idd kwa amani na utulivu huku akiwahimiza kujitolea kwa watu wenye uhitaji, hususan katika siku hii muhimu.

Katika hotuba yake, Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga, Soud Kategile, amewakumbusha waumini kuhusu umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ambapo amehimiza kuchagua viongozi bora na kuepuka vitendo vya rushwa katika kipindi hicho.

Baadhi ya waumini waliohudhuria ibada hiyo wameahidi kuzingatia maelekezo ya viongozi wao kwa ajili ya kuendeleza amani, mshikamano na maendeleo ya jamii.

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, akiongoza ibada ya swala ya Eid Al Fitr leo Machi 31, 2025 katika uwanja wa Sabasaba Kambarage Mjini Shinyanga.

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, akiongoza ibada ya swala ya Eid Al Fitr leo Machi 31, 2025 katika uwanja wa Sabasaba Kambarage Mjini Shinyanga.




 

Post a Comment

Previous Post Next Post