" WANANCHI WAMPONGEZA SAGINI KWA UFUATILIAJI WA MIKOPO YA HALMASHAURI

WANANCHI WAMPONGEZA SAGINI KWA UFUATILIAJI WA MIKOPO YA HALMASHAURI


Wananchi wa Kijiji cha Kisamwene Kata ya Butuguri wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Butiama ambaye pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini kwa ufuatiliaji wake mpaka kufanikisha kupata mikopo ya Vikundi vya wajasiliamali inatolewa na Halmshauri asilimia 10 kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.

Mhe. Sagini amepewa pongezi hizo katika   Ziara yake ya Kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwenye Vijiji vya Kibubwa, Kisamwene na Busirime vilivyopo Kata ya Butuguri, Wilaya ya Butiama mkoani Mara. Machi 17, 2025 ambapo Diwani wa Kata ya Butuguri Mhe. Paul Meha kwa niaba ya wananchi amekiri vikundi vya kijiji himo kupokea mikopo baada ya Mbunge kufuatilia kwani awali walikuwa wakikosa.

Pia Mbunge wa Jimbo la Butiama ambaye pia ni Naibu Waziri Katiba na Sheria amesema kuwa huo mwendelezo wa juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwakwamua wananchi kiuchumi kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani yanayotengwa kwa ajili ya kuinua kipato cha makundi hayo.

Mbunge Sagini ametaka wanufaika wa mikopo isiyo na riba wakaendeleze shughuli za ujasiliamali kama walivyoeleza katika maandiko waliyowasilisha wakati wa maombi ya mkopo ili waweze kujikwamua kiuchumi ili kuchangia pato la taifa.

Hata hivyo baadhi ya wanufaika kutoka vikundi vya Juhudi, Tujikomboe na Tupendane wamesema wa mikopo hiyo waliopata kwa ufuatiliaji wa Mbunge Sagini italeta unafuu kutokana na masharti yake hasa ikilinganishwa na mingine hasa inayotolewa na baadhi ya taasisi binafsi.












Post a Comment

Previous Post Next Post