" WAZIRI PEMBE JUMA AKEMEA UKATILI ASISITIZA USAWA KWA WANAWAKE WENYE ULEMAVU, SMAUJATA YAHIMIZA WANAWAKE WENYE ULEMAVU KUSHIRIKISHWA KATIKA UONGOZI NA MAENDELEO

WAZIRI PEMBE JUMA AKEMEA UKATILI ASISITIZA USAWA KWA WANAWAKE WENYE ULEMAVU, SMAUJATA YAHIMIZA WANAWAKE WENYE ULEMAVU KUSHIRIKISHWA KATIKA UONGOZI NA MAENDELEO

Mgeni rasmi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wanawake na Wanawake wenye ulemavu Mkoani Shinyanga leo Machi 1, 2025. 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA), Idara ya Wenye Ulemavu, imeadhimisha siku ya Wanawake na Wanawake wenye ulemavu Mkoani Shinyanga  kwa lengo la kusisitiza mchango wa wanawake wenye ulemavu katika maendeleo ya jamii na kupambana na changamoto wanazokutana nazo.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma, ambapo amepongeza wanawake wenye ulemavu kwa bidii yao katika kuchangia maendeleo ya jamii na kuwataka wadau mbalimbali kushirikiana kuhakikisha kundi hilo linapata nafasi sawa katika sekta zote.

"Siku ya Wanawake Duniani ni fursa ya kutambua mchango wa wanawake wote, wakiwemo wenye ulemavu, katika maendeleo ya taifa. Ni jukumu letu kuhakikisha wanapata haki zao na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi," amesema Mhe. Riziki.

Amepongeza juhudi za wanawake wenye ulemavu katika kuchangia maendeleo ya jamii licha ya changamoto wanazokumbana nazo.

"Siku ya Wanawake Duniani ni alama muhimu ya kutambua mchango wa wanawake wote, bila kujali hali zao. Tunapaswa kuhakikisha kuwa wanawake wenye ulemavu wanapata nafasi sawa katika elimu, ajira na uongozi, ili wawe sehemu ya maendeleo ya nchi," amesema.

Ameongeza kuwa serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuboresha huduma za jamii kwa wanawake wote, ikiwemo upatikanaji wa elimu, huduma za afya na maji safi, ili kuhakikisha wanapata mazingira bora ya maisha.

Amewahimiza wanawake  kujikita katika malezi bora ya watoto wao, kwani wao ndio viongozi wa kesho huku akisisitiza  kutumia nafasi waliyonayo kuhamasisha vijana kuhusu umuhimu wa kusimamia misingi ya maadili, ili kujenga kizazi chenye uwajibikaji.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa, Shujaa Sospeter Mosewe Bulugu, amesema kuwa SMAUJATA imeanzishwa ili kuchochea shughuli za maendeleo na ustawi wa jamii, huku akibainisha kuwa SMAUJATA ilizinduliwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, mnamo Juni 16, 2022.

"Dira ya SMAUJATA ni kuwa na taifa lenye kizazi huru chenye haki na usawa kitakachoweza kujitegemea na kuzitambua fursa na kutumia ujuzi, maarifa na vipaji katika kujenga jamii yenye maendeleo endelevu," amesema Bulugu.

Akisoma risala Katibu wa Idara ya Wenye Ulemavu SMAUJATA Taifa, Imani Axwesso, ambaye ameainisha changamoto zinazowakabili wanawake wenye ulemavu, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira, mitaji ya biashara, mikopo, na nafasi za uongozi.

"Jamii inapaswa kuhakikisha kuwa mwanamke mwenye ulemavu anashirikishwa kikamilifu katika nafasi mbalimbali za kimaendeleo ili aweze kujitegemea, lakini pia ashiriki katika maamuzi muhimu ya uongozi," amesema Axwesso.

Ametaja changamoto zinazowakabili wanawake wenye ulemavu ikiwemo ukatili wa kijinsia, unyanyapaa, na ubaguzi katika jamii huku akihimiza  serikali na wadau wa maendeleo kuweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha kiuchumi na kuhakikisha wanapata huduma bora za elimu na afya.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, ameipongeza SMAUJATA kwa juhudi zake za kupambana na ukatili dhidi ya wanawake wenye ulemavu, akisema kuwa juhudi hizo zimechangia kupunguza matukio ya ukatili katika mkoa huo.

Maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu: "WANAWAKE NA WASICHANA 2025 TUIMARISHE HAKI, USAWA NA UWEZESHAJI." Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha jamii kutambua uwezo wa wanawake wenye ulemavu na kuwajumuisha katika ajira, elimu na fursa nyingine za maendeleo.

SMAUJATA inatoa wito kwa serikali, taasisi binafsi na jamii kwa ujumla kuungana pamoja kuboresha hali za wanawake wenye ulemavu.

Mgeni rasmi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wanawake na Wanawake wenye ulemavu Mkoani Shinyanga leo Machi 1, 2025. 

Mgeni rasmi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wanawake na Wanawake wenye ulemavu Mkoani Shinyanga leo Machi 1, 2025.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya Wanawake na Wanawake wenye ulemavu Mkoani Shinyanga  leo Machi 1, 2025.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya Wanawake na Wanawake wenye ulemavu Mkoani Shinyanga  leo Machi 1, 2025.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa, Shujaa Sospeter Mosewe Bulugu, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya Wanawake na Wanawake wenye ulemavu Mkoani Shinyanga  leo Machi 1, 2025.

Katibu wa Idara ya Wenye Ulemavu SMAUJATA Taifa, Imani Axwesso, akisoma risala kwenye maadhimisho hayo ya Wanawake na Wanawake wenye ulemavu Mkoani Shinyanga  leo Machi 1, 2025.




Post a Comment

Previous Post Next Post