" WILAYA ZA URAMBO NA KALIUA KUPATA UMEME WA UHAKIKA BAADA YA KITUO CHA KUPOZA UMEME KUKAMILIKA

WILAYA ZA URAMBO NA KALIUA KUPATA UMEME WA UHAKIKA BAADA YA KITUO CHA KUPOZA UMEME KUKAMILIKA



 Na Lucas Raphael,Tabora

WILAYA ZA URAMBO NA KALIUA KUPATA UMEME WA UHAKIKA BAADA YA KITUO CHA KUPOZA UMEME KUKAMILIKA .

 

SHIRIKA la umeme Tanzania Tanesco mkoani wa Tabora kwa kushirikiana na Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme ( ETDCO) imefanikiwa kuwasha rasmi laini ya msongo wa Kilovolti 132 yenye mrefu wa kilomita 115 kutoka Tabora mjini hadi wilayani urambo mkoani Tabora   .

Kuwashwa kwa umeme huo utasaidia  wananchi wa Urambo na Kaliua kupata umeme wa uhakika na kuchochea vyanzo vya uchumi na kuwaletea maendeleo.

Kaimu mkurugenzi wa huduma za ufundi kutoka kampuni tanzu ya shirika la umeme Tanzania Tanesco ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme ambao ndio wanaotekeleza mradi huo chini ya usimamizi wa Tanesco  Mhandisi. Dismas Masawe  alisema ukamilishaji wa umeme kutoka hapa tabora mjini hadi kituo cha kupoza umeme cha Uhuru wilayani urambo kupata umeme wa uhakika .

Alisema kwamba wameunganisha mifumo ya umeme kwa asilimia 100 baada ya kuchaji mfumo huo kutoka laini ya Msongo wa    kilovoti 132 kutoka Tabora mjini hadi wilaya ya Urambo mkoani hapa.

Alifafanua kwamba Wananchi wa wilaya za Urambo na Kaliua kila moja watakuwa wanapata umeme wa uhakika na watakuwa na laini yao pekee tofauti na zamani ambao walikuwa wanapata umeme kutoka Tabora mjini  kwenda Urambo wakichangia na wilaya ya Kaliua na Uyui.

Kaimu meneja  mkuu wa ETDCO Cpa Sadock Mugendi  aliwataka wakazi wa mkoa wa Tabora kutunza miundombinu ya ujenzi huo ili iliweze kutumika kwa muda mrefu .

 

Alisema wananchi ambao miundombinu inakopita ndio wanatakiwa kuwa walinzi wa rasilimali hiyo ambayo serikali imewekeza fedha nyingi kwa ajili ya kuwapatia umeme wananchi wa mkoa wa Tabora na viunga vyake.

 

“Leo hii tuweze kufanya majaribio ya kuunga umeme kutoka kituo kikuu cha umeme cha Tabora mjini hadi kituo cha umeme cha uhuru wilayani Urambo mkoani hapa

 

Alisema awali wilaya ya urambo walikuwa wakipata umeme wa Msongo wa kilovoti 33 lakini sasa wapata umeme wa Msongo wa kilovoti 132 ambao ni umeme wa kutosheleza mahaitaji .

 

Cpa Sadock Mugendi aliwataka wananchi wote walipisha maeneo yao na kulipwa fidia na serikali wasirudi tena maeneo hayo kwa ajili yakuendelea shughuli za kibinadamu  kwani tayari walishalipwa lakini sasa wanarudi tena kuendelea na kilimo jambo ambalo litadhiri miundombinu hiyo ya umeme.

 

Hata hivyo  Meneja Mradi wa njia ya msongo wa kilovoti 132 kutoka Tabora hadi wilaya ya urambo Mhandisi Sospeter Ulalo alisema mradi wa ujenzi umetumia kiasi cha shilingi bilioni 40 hadi kukamilika kwake .

 

Alisema kwamba njia ya kusafirishia umeme imetumia kiasi cha shilingi billion 24 na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha uhuru wilayani Urambo kimetumia kiasi cha shilingi  billion 16 kwa umbali wa kilometa 115.

 

Alibainisha kuwa mradi huo umefanikiwa kwa asalimia 100 na hivyo wananchi wa wilaya ya Urambo na Kaliua tayari kupata uemem wa uhakika .

 

Alisema kwamba umeme huo kila wilaya itakuwa na njia yake kwa ajili ya wilaya ya urambao ikipata Itilafu haitadhiri wilaya nyingine kuendelea kupata umeme kila wilaya itakwa na njia inayojitengemea ua umeme maana tuna sema kutakuwa na umeme wa uhakika.

 

Ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Uhuru wilayani urambo na ujenzi wa laini kubwa ya kusafirishia umeme wa Msongo wa kilovoto 132 kutoka Tabora hadi urambo ulianza machi mwaka 2024 na kumalikazi juni  mwaka huu 2025 ila umweza kumaliza mapema kabla ya mwezi huo

 

“Tunashukuru Mungu tumefanikiwa kumaliza mradi huu kabla ya wakati ili wananchi wa Urambo waweze kupata umemea mapema'alisema 

Fundi akikamilisha taratibu wa kuwasha umeme kutoka kituo kikuu cha Tabora mjini kwenda wilaya urambo mkoani hapa

Post a Comment

Previous Post Next Post