" 19 MBARONI KWA TUHUMA ZA KUFUNDISHA VIJANA MBINU ZA KUWA MABILIONEA

19 MBARONI KWA TUHUMA ZA KUFUNDISHA VIJANA MBINU ZA KUWA MABILIONEA

 !9 Mbaroni Kwa Tuhuma za Kufundisha Vijana Mbinu za Kuwa Mabilionea



Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu 19 wanaodaiwa kuwa matapeli kutoka katika makampuni yanayowarubuni vijana kwa kuwafundisha mbinu za utajiri kupitia njia za mtandaoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amesema kuwa makampuni hayo yamekuwa yakiwaingiza vijana katika mipango isiyo halali ya kupata utajiri, na kwa sasa jeshi hilo linafanya uchunguzi kubaini uhalali wa shughuli zao.

Aidha, Mkama amebainisha kuwa katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu, jumla ya vijana 399 wameokolewa kutoka mikononi mwa watu hao waliokamatwa.

Jeshi la Polisi limewataka vijana kuwa makini na matangazo yanayoahidi utajiri wa haraka, huku likiendelea na uchunguzi zaidi juu ya suala hili.

Post a Comment

Previous Post Next Post